Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Mtumishi wa umma aliyepata ajali, kuumia au kufariki akiwa kazini anatakiwa atoe taarifa kwa mwajiri wake kisha mwajiri afuate taratibu zifuatazo:-
•Mwajiri anapaswa kuwasilisha taarifa ya awali kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma huku akiendelea kuunda kamati ya uchunguzi wa ajali Kanuni 111(1) na 111(2) yahusika.
•Baada ya kamati ya uchunguzi kukamilisha taarifa, mwajiri anapaswa kuwasilisha taarifa hiyo kwa Katibu Mkuu (Utumishi) ikiwa na mapendekezo yake mintaarafu Kanuni 111(5).
•Katibu Mkuu – Utumishi atawasilisha mapendekezo yote pamoja na ushauri wake kwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kuamua kiwango cha malipo ya fidia kwa mtumishi aliyepata ajali akiwa kazini hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 112.
Ili kuongeza uwajibikaji, kila Taasisi ya Umma inatakiwa iwe na Mkataba wa Huduma kwa Mteja.Mkataba wa Huduma kwa Mteja unawapa fursa wateja kuelewa ubora wa huduma zinazotolewa na taasisi za umma. Kimsingi,na kwa kuwa kila Wizara kwa sasa tayari ina mfumo wa utendaji wa kimenejimenti ambayo mojawapo ya mahitaji ni kuwa na mkataba wa huduma kwa mteja
Suala la ajira mpya linategemea na kuwepo kwa mahitaji halisi ya kuwa na mtumishi mpya na inatakiwa kuingizwa kwenye bajeti (Ikama).Nafasi ambazo ziko wazi kabla ya kujazwa lazima fedha itengwe (Bajeti) kwa ajili ya watumishi watakaoajiriwa.Jukumu hili ni la mwajiri mwenyewe ambaye anawajibu wa kuangalia maeneo yanayohitaji rasilimali watu.Hata hivyo,kama zilivyo nafasi za ajira mbadala,kwa nafasi mpya pia ni lazima zipatiwe vibali vya ajira mbadala,kwa nafasi mpya pia ni lazima zipatiwe vibali vya ajira pamoja na kufuatwa kwa taratibu za ajira kwa mujibu wa Sera ya Menejimenti na Ajira ya mwaka 1999 na Sheria ya Utumishi wa Umma Na.8 ya mwaka 2002 pamoja na marekebisho yake Na.17 ya mwaka 2007.
Iwapo mtumishi wa umma ambaye hajaridhika na adhabu aliyopewa iliyotokana na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa utaratibu ulio rasmi na ule usio rasmi anaweza kukata rufaa kama ilivyoonyeshwa katika Jedwali lililotangulia.
Katika Utumishi wa Umma zipo aina mbili za ushughulikiwaji wa makosa ya kinidhamu. Aina hizo ni:-
(i)Makosa yanayoshughulikiwa kwa utaratibu rasmi (formal proccedings)-Kanuni 42(1) Kanuni za Utumishi wa Umma,2003
(ii)Makosa yanayoshughulikiwa kwa utaratibu usio rasmi(summary proceedings-Kanuni 43(1), Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003
•Makosa yanayofaa kushughulikiwa kwa utaratibu ulio rasmi pamoja na adhabu zimeorodheshwa katika Jedwali la Kwanza, Sehemu ‘A’ ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003
•Makosa yanayofaa kushughulikiwa kwa utaratibu usio rasmi pamoja na adhabu zimeorodheshwa katika Jedwali la Kwanza, Sehemu B, Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003
Mamlaka ya kulipa fidia itatoa taarifa ya kiwango cha fidia kwa mwajiri na endapo fidia husika imeridhiwa, mwajiri wa mtumishi atapaswa kuandaa malipo hayo na pale mwajiri anaposhindwa kulipa fidia husika anaweza kuwasilisha maombi hayo Hazina.
Mwajiri ambaye hataridhika na uamuzi uliotolewa na mamlaka ya rufaa anaweza kukata rufaa kwa mamlaka ya juu ya rufaa inayostahiki.
Sio kweli kuwa kwenye mfumo wa Utumishi watu wenye elimu ndogo ndio wanaopangwa vijijini.Utaratibu uliopo ni wa kuhakikisha kuwa watumishi wanapangwa sehemu mbalimbali za nchi kulingana na mahitaji.
Ili mtumishi wa umma aweze kulipwa mshahara binafsi inatakiwa apate kibali cha mshahara binafsi kinachotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma mintaarafu mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 Kifungu Na. 8 (3) (e) kikisomwa kwa pamoja na Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma Toleo la Mwaka 2009 Kanuni E.1.
Taratibu zinazotumika kumpandisha cheo mtumishi wa umma zimeainishwa katika Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma ya mwaka 2008 ikisomwa kwa pamoja na Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003 kama ifuatavyo:-
i) Kuwepo kwa nafasi iliyotengewa fedha katika mwaka wa fedha husika,
ii) Muundo wa utumishi (scheme of service) wa kada husika,
iii) Utendaji mzuri wa kazi,
iv) Orodha ya ukubwa kazini (seniority list),
v) Maendeleo ya kitaaluma (career development),
vi) Urithishanaji wa madaraka (succession plan).