Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma (ina utaratibu wa kuwahimiza waajiri wote kama:Wizara,Idara Zinazojitegemea,Wakala na Sekretarieti za Mikoa kutunza kumbukumbu za watumishi ambao wako masomoni na watakaokuwa masomoni na kuwasilisha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kila mwaka wa fedha kupitia miongozo na nyaraka mbalimbali ikijumuisha mipango na mahitaji ya mafunzo ya kila taasisi.Aidha, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ina utaratibu wa kuhifadhi kumbukumbu kwa watumishi ambao wako masomoni nje ya nchi.Utaratibu huu unaendelea kuboreshwa kwa kuwatambua watumishi ambao hawarejei nyumbani mara baada ya kumaliza masomo yao kwa kushirikiana na waajiri.

Gazeti la Serikali ni kielelezo muhimu kwa wadau mbalimbali hapa nchini katika utendaji kazi, hivyo ni vema waajiri na wananchi wakawasilisha taarifa zao muhimu ili ziweze kuchapishwa kwenye Gazeti ili zitumike kama marejeo katika utatuzi wa migogoro ikiwemo ya ardhi na kuwezesha kufanya maamuzi muhimu ya kiutendaji.

Waajiri katika Taasisi za Umma wanatakiwa kuwasilisha taarifa za kiutumishi zinazopaswa kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali kwa njia ya nakala ngumu (hard copy) na nakala laini (soft copy).Aidha, taarifa zinazowasilishwa na watu binafsi kwa ajili ya kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali zinatakiwa kuwasilishwa kwa njia ya nakala ngumu (hard copy)

Gazeti la Serikali linapatikana kwenye Ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali iliyopo eneo la Uhindini jijini Dodoma. Aidha, unaweza kulipata katika Maktaba ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa ajili ya rejea.

Kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma toleo la mwaka 2009 Kifungu C. 27, Gazeti la Serikali linapaswa kuchapishwa kila Ijumaa ya wiki baada ya taarifa zinazowasilishwa na wadau kuhaririwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na kupelekwa kwa Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kila Jumanne ya wiki.

Hakuna gharama yoyote kwa matangazo yanayowasilishwa na Taasisi za Serikali kwa ajili ya kuchapishwa katika Gazeti la Serikali.Kwa upande wa matangazo yanayowasilishwa na watu binafsi itawalazimu kulipa kiasi cha shilingi 20,000/= kwa Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kupitia namba ya malipo (Control Number) ili tangazo lake lipate uhalali wa kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali.

Matangazo yote ya Serikali pamoja na ya watu binafsi yanayotakiwa kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali huwasilishwa kwa Mhariri wa Gazeti la Serikali ambaye ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa ajili ya kuhaririwa. Mara baada ya matangazo hayo kuhaririwa huwasilishwa rasmi kwa Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali.

 
 • Muundo wa Serikali na Majukumu ya Wizara

 • Sheria ndogondogo za halmashauri

 • Uteuzi wa wajumbe wa baraza la ardhi

 • Usajili wa vyama vya wafanyakazi

 • Mali isiyo na mwenyewe na;

 • Kufutwa kwa kampuni 


 • Kupotea kwa hati ya usimamizi wa ardhi

 • Usimamizi wa Mirathi

 • Mali iliyopotea (Loss report)

 • Kubadili jina (Deed poll)

 • Kufunga Kampuni

Taarifa za kiutumishi zinazopaswa kuchapishwa katika Gazeti la Serikali ni za;
 • Kuajiriwa na kukabidhiwa madaraka

 • Kuthibitishwa kazini

 • Kuacha kazi

 • Kufukuzwa kazi

 • Kustaafu na;

 • Tanzia