Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Taarifa za kiutumishi zinazopaswa kuchapishwa katika Gazeti la Serikali ni za;




  • Kuajiriwa na kukabidhiwa madaraka

  • Kuthibitishwa kazini

  • Kuacha kazi

  • Kufukuzwa kazi

  • Kustaafu na;

  • Tanzia

Kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma (Government Standing Orders) toleo la mwaka 2009 Kifungu C. 27 hadi C.30, ni muhimu kwa kila taasisi ya Serikali kuwasilisha taarifa mbalimbali za kiutumishi kwa ajili ya kutangazwa katika Gazeti la Serikali kwani hutumika kama marejeo katika kufanya maamuzi muhimu kwa mfano mtumishi akipoteza barua ya kuajiriwa (first appointment) huweza kutumia nakala ya Gazeti la Serikali lililochapisha taarifa zake kuthibitisha ajira yake.

Lengo la kuanzishwa kwa Gazeti la Serikali ni kuchapisha na kuhifadhi taarifa muhimu zitakazotumika kama marejeo katika kutatua migogoro au kufanya maamuzi muhimu kwani matangazo ya gazeti la Serikali yanapochapishwa huwa rasmi kwa utekelezaji hapa nchini.

Gazeti la Serikali lilianzishwa kwa mujibu wa “General Orders” kifungu C.56- C.62 ya mwaka 1957 pamoja na marekebisho yake katika Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Kifungu C.28-C.30 toleo la mwaka 1971, Kifungu C.28-C.31 toleo la mwaka 1994 na Kifungu C.27-C.30 toleo la mwaka 2009. Gazeti hili linategemewa katika kufanya maamuzi mbalimbali yakiwemo ya kisheria.

Gazeti la Serikali ni kielelezo muhimu cha taarifa za Serikali, taasisi binafsi, wananchi na wadau mbalimbali zinazotumika katika utendaji wa kila siku.