Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Kuhusu Sisi

1.0  UTANGULIZI

Jukumu kubwa la OR-MUUUB ni kuimarisha Utawala Bora katika uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa kubuni Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu za uendeshaji na usimamizi wa shughuli za utumishi wa umma na kujenga uwezo wa watumishi wa Umma ili watoe huduma bora kwa  wananchi. Kwa mujibu wa Hati ya Mgawanyo wa Majukumu kwa Mawaziri kama ilivyotangazwa katika Gazeti la Serikali Toleo Na. 619A&619B la tarehe 30/8/2023, OR-MUUUB ina majukumu yafuatayo:-

 1. Kuandaa, kuhuisha na kusimamia utekelezaji wa Sera za Utawala, Serikali Mtandao, Makazi ya Watumishi wa Umma, Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma;
 2. Kusimamia Utawala wa Utumishi wa Umma;
 3. Kusimamia mikataba ya utendaji kazi Serikalini;
 4. Kusimamia mipango na uendelezaji rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma;
 5. Kusimamia Orodha ya Mishahara katika Utumishi wa Umma;
 6. Kusimamia Maadili ya Utumishi wa Umma;
 7. Kuandaa na kusimamia miundo na mifumo ya uendeshaji wa Serikali na uboreshaji wa utoaji huduma wa Utumishi wa Umma;
 8. Kuratibu uanzishwaji na uendelezaji wa Wakala za Serikali;
 9. Kusimamia na maboresho katika Utumishi wa Umma;
 10. Kusimamia utendaji kazi na uendelezaji wa rasilimaliwatu katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma; na
 11. Kusimamia taasisi, programu na miradi iliyo chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

1.1 DIRA NA DHIMA

1.1.1 DIRA

Kuwa na “Utumishi wa umma wenye ufanisi na uwajibikaji katika kufikia ustawi wa Taifa"

1.1.2 DHIMA

“Kusimamia utumishi wa umma kupitia Sera, Mifumo na Miundo ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu iliyoboreshwa”

1.2  Maadili ya Msingi katika Taasisi

-Uzalendo

-Uadilifu

-Ubora 

-Mteja Kwanza