English | Swahili

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAFANYA UFUATILIAJI WA UTEKELEZAJI WA WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WAKE

Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Ukuzaji Maadili, Sehemu ya Ufuatiliaji Uzingatiaji wa Maadili, Bibi Janeth Mishinga akihimiza uzingatiaji wa Waraka wa Mavazi Na. 3 wa Mwaka 2007 kwa watumishi wa Umma  nchini mara baada ya kukamilika kwa zoezi la ukaguzi na ufuatiliaji wa Waraka huo kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.


Read More...

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAFANYA UFUATILIAJI WA UTEKELEZAJI WA WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WAKE

Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Ukuzaji Maadili, Sehemu ya Ufuatiliaji Uzingatiaji wa Maadili, Bibi Janeth Mishinga  akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Uadilifu wa ofisi hiyo wakati wa zoezi la ukaguzi na ufuatiliaji wa Waraka wa Mavazi Na. 3 wa Mwaka 2007 lililofanyika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa lengo la kuhimiza uzingatiaji wa waraka huo kwa watumishi wa umma nchini.


Read More...

SERIKALI YAELEKEZA KUSIMAMISHWA KAZI MKUU WA IDARA YA UTAWALA NA UTUMISHI WA MANISPAA YA ILALA NA KUWACHUKULIA HATUA ZA KINIDHAMU WATUMISHI WENGINE WA MANISPAA HIYO

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ofisini kwake jijini Dodoma leo kuhusu kusimamishwa kazi kwa Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi wa Manispaa ya Ilala Bi. Benadeta Mwaikambo na kuwachukulia hatua za kinidhamu maofisa wanaohusika na Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu.


Read More...

TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUZINGATIA USALAMA WA TAARIFA KATIKA UTEKELEZAJI WA SERIKALI MTANDAO

Baadhi ya Watendaji Wakuu wa Taasisi serikalini wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma. 


Read More...

TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUZINGATIA USALAMA WA TAARIFA KATIKA UTEKELEZAJI WA SERIKALI MTANDAO

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao, Dkt. Jabiri Bakari akizungumza kabla ya ufunguzi wa kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma.


Read More...

TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUZINGATIA USALAMA WA TAARIFA KATIKA UTEKELEZAJI WA SERIKALI MTANDAO

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akifungua rasmi kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao kilichowajumuisha Watendaji Wakuu Serikalini katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma.


Read More...

TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUZINGATIA USALAMA WA TAARIFA KATIKA UTEKELEZAJI WA SERIKALI MTANDAO

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge akiwakaribisha katika mkoa wake wajumbe wa kikao kazi cha pili cha  Serikali Mtandao kabla ya kuanza kwa kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma.


Read More...

SERIKALI MTANDAO YARAHISISHA UPATIKANAJI WA HUDUMA KWA WANANCHI KWA WAKATI

Mkurugenzi Idara ya Ushauri na Uchambuzi Kazi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba akifungua rasmi kikao kazi cha Serikali Mtandao kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma.


Read More...

SERIKALI MTANDAO YARAHISISHA UPATIKANAJI WA HUDUMA KWA WANANCHI KWA WAKATI

Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Serikali Mtandao wakimsikiliza Mkurugenzi Idara ya Ushauri na Uchambuzi Kazi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma.


Read More...

SERIKALI MTANDAO YARAHISISHA UPATIKANAJI WA HUDUMA KWA WANANCHI KWA WAKATI

Mkurugenzi Idara ya TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Priscus Kiwango akitoa neno la shukrani na kuahidi kutekeleza maelekezo ya mgeni rasmi baada ya ufunguzi wa kikao kazi cha Serikali Mtandao katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma mapema leo.


Read More...
Wasiliana na Dawati la Msaada Kupitia namba hizi 0682-800-999/ 0620464042 na barua pepe dawatilamsaada@utumishi.go.tz

News and Events

Quick Links

1611156
TodayToday2660
YesterdayYesterday2733
This_WeekThis_Week3291
This_MonthThis_Month57711
All_DaysAll_Days1611156

social media button generator

Location Map

Quick Contacts

Phone:+255 (026) 2963630
Fax:+255 (026) 2963629
Email :ps@utumishi.go.tz
Website:http://www.utumishi.go.tz

Site Poll

How do you rate our services?