Taasisi za Umma nchini zatakiwa kuwapatia huduma ya usafiri Watumishi wa Umma wenye ulemavu

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Amina S. Mollel  Bungeni leo jijini Dodoma, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililohusu  mpango  wa Serikali wa kuwapatia huduma ya usafiri Watumishi wa Umma wenye Ulemavu.