Serikali yawataka maafisa ugani nchini kutoa huduma ya kitaalamu kwa wananchi kuleta matokeo chanya

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ambaye ni Mgeni Rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani Kagera akitunuku cheti na zawadi kwa watumishi wa Kiwanda cha Sukari Kagera ambao ni washindi wa pili wa jumla wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima katika Viwanja vya Kyakailabwa mkoani Kagera.