Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akikabidhiwa tuzo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene na Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) Mkoani Iringa mara baada ya kufungua Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa 54 wa Chama Cha Wauguzi Tanzania unaofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo kukiwa na jumla ya Washiriki 1500.