Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Uongozi

Utawala wa Jamhuri ya Muungano una Rais, Makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar, Waziri wa Mkuu na Baraza la Mawaziri.

Rais wa Jamhuri la Muungano ndiye Mkuu wa nchi, Mkuu wa Serekali, Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi.

Rais ndiye kiongozi wa Utawala wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Makamu wa Rais ndiye msaidizi mkuu wa Rais kwa mambo yote ya Jamhuri ya Muungano  kwa ujumla na hasa ana wajibu wa kumsaidia Rais katika;

i. Kufuatilia utelekezaji wa kila siku wa mambo ya muungano

ii. Kufanya kazi zote atakazopewa na Rais

iii. Kufanya kazi zote na majukumu ya ofisi ya Rais, wakati Rais asipokuwepo au anapokuwa nje  ya nchi

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ndiye Kiongozi wa shughuli za Serekali  Bungeni na ana mamlaka ya kudhibitisha, kusimamia na kutelekeza kazi za kila siku na mambo ya Serekali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha anatekeleza jambo lolote ambalo Rais atamwelekeza kuwa lifanywe.

Rais wa Zanzibar ndiye Kiongozi wa Utawala wa Zanzibar, Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar

Baraza la Mawaziri ni pamoja na Waziri Mkuu, anayeteuliwa na Rais kutokana na Wabunge wa Bunge la Taifa. Serekali inatekeleza kazi zake kupitia kwa Wizara zinazoongozwa na Mawaziri. Kila wizara ina dhmana ya kazi na sekta yake.