Habari
WAZIRI MHE. SIMBACHAWENE AZITAKA TAASISI ZA UMMA KUZINGATIA MIKATABA YA HUDUMA KWA MTEJA KATIKA KUTOA HUDUMA BORA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akifurahia jambo na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw.Juma Mkomi wakati wa Uzinduzi wa Mikataba ya Huduma kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.