Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

WAZIRI SIMBACHAWENE ATOA RAI KWA WANANCHI KUTUMIA MIFUMO YA TEHAMA YA SERIKALI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ametoa rai kwa  wananchi kuwa wafuatilliaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika simu zao za kiganjani ili kujipatia  huduma nyingi za kijamii zitolewazo na Serikali

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Julai 19, 2024 wakati akifungua Maadhimisho na Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza Juni 16 katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Mhe.Simbachawene amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza matumizi ya TEHAMA katika kuwawezesha wananchi kupata huduma zitolewazo na Serikali kwa haraka, uwazi na bila kuwa na urasimu

Kufuatia hatua hiyo amesisitiza wananchi kutumia simu zao ili kupata huduma hizo badala ya kujikita kuangalia pekee michezo ya kubashiri na tamthilia kupitia simu zao za kiganjani

Amesema lengo la kuhakikisha huduma za serikali zinapatikana kupitia simu za kiganjani ni kuona wananchi wanapata huduma bora zenye gharama nafuu na kwa haraka katika mikoa na wilaya zote tofauti ilivyokuwa miaka ya nyuma  

Wakati huo huo, Mhe.Simbachawene amewataka Watumishi wa Umma kutumia mifumo ya TEHAMA iliyobuniwa na Serikali ili kurahisisha utoaji huduma na kuondoa malalamiko kwa wananchi wanaowahudumia

Katika hatua nyingine Mhe. Simbachawene amewataka watumishi ambao hawajajisajili na kujaza mipango kazi katika Mfumo wa Upimaji wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma (PEPMIS) wawe wamekamilisha kabla ya wiki ijayo ili kila mmoja awe ameingia kwenye mfumo huo.

 

“Kabla sijahitimisha hotuba yangu nitoe maelekezo yafuatayo, Watendaji wote wahakikishe watumishi ambao bado hawajajisajili kwenye Mfumo wa Upimaji wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma (PEPMIS) wawe wamefanya kazi hii ili mpaka wiki ijayo jambo hili liwe limeshakwisha kabisa na kila mmoja awe ameingia kwenye mfumo.” Amesema Mhe

 Mhe. Simbachawene

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kitaifa yanaratibiwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo kwa mwaka huu, Wizara na Taasisi mbalimbali za serikali zinatoa huduma za papo kwa hapo ikiwemo  hati za viwanja, vitambulisho vya uraia  na huduma nyinginezo katika Viwanja vya Chinangali Park.