Habari
WAZIRI SIMBACHAWENE AFANYA KIKAO KAZI NA WATUMISHI WA SEKRETARIETI YA MAADILI NA KUKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO JIPYA LA OFISI HIYO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (katikati) akizungumza jambo na Naibu Waziri wake Mhe. Ridhiwani Kikwete (Wa kwanza kushoto) mara baada ya kukagua jengo jipya la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma, Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi.