Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Walimu pamoja na Maafisa Utumishi wakati akifunga mafunzo ya siku tatu yaliyofanyika jijini Dodoma kuhusu Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) utakaosaidia kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili Walimu nchini.