Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

WAZIRI MHE.SANGU : MFUMO WA UPIMAJI UTENDAJI KUJAZWA KILA WIKI NA WATUMISHI NA SIO VINGINEVYO 


Naibu Waziri,  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Mhe. Deus Sangu amesema Mfumo  wa upimaji wa utendaji kazi kwa Watumishi wa Umma ujulikanao kama PEPMIS utaendelea kujazwa kwa wiki kama ilivyopangwa.

Mhe. Deus Sangu amesema hayo Bungeni leo Jummane Januari 29, 2025 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Sophia Mwakagenda aliyetaka kujua kwa nini watumishi wa afya wasijaze ripoti za utendaji kila mwezi badala ya kila wiki ili wapate muda zaidi kuhudumia wagonjwa