Habari
WATUMISHI WAASWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU WANAPOTIMIZA WAJIBU WAO
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imewataka Watumishi wa Umma kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu huku wakisistizwa kutambua haki zao za msingi wanazostahili kama Watumishi wa Umma.
Mkuu, Bw. Elibariki Funga akiwasilisha mada kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Desemba 23, 2024 katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma wakati akitoa mafunzo ya haki na wajibu kwa Watumishi wa Umma nchini, ikiwa ni muendelezo wa kutoa mafunzo elekezi ya kila wiki kwa Watumishi hao kwa lengo la kuboresha utendaji kazi kwa Watumishi wa Umma nchini.
Amesema ni wajibu wa kila Mtumishi kutambua haki zake ikiwemo stahili zake kama Mtumishi wa Umma pamoja na likizo huku akisisitiza haki lazima iende sambamba na kutimiza wajibu wa kutoa huduma bora kwa wananchi.
Amesema endapo Watumishi wa Ofisi hiyo wataweza kufahamu vizuri haki zao wataweza kuwajibika ipasavyo ili kuendana na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.