Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

WATUMISHI WA OFISI YA RAIS-UTUMISHI WAUNGANA NA WAFANYAKAZI DUNIANI KUADHIMISHA SIKU YAO ADHIMU


Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wameungana na Wafanyakazi Duniani kote leo Mei Mosi, 2024 kuadhimisha siku yao Adhimu ambapo nchini Tanzania, Kilele cha Siku hiyo Kitaifa imefanyika jijini Arusha na Mgeni Rasmi wa Sherehe hizo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango.

Kaulimbiu ya siku hii ya Wafanyakazi Duniani kwa mwaka huu ni “Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha”

Aidha, kwa upande wa Utumishi wa Umma ulibeba kaulimbiu isemayo “Utumishi wa Umma Ulioboreshwa ni Chachu ya Utendaji Kazi Unaozingatia Haki na Wajibu”.