Habari
WATUMISHI WA OFISI YA RAIS-UTUMISHI WAPIMA AFYA KWA HIARI

Watumishi wa Umma wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wameitikia wito wa kushiriki zoezi muhimu la upimaji wa afya wa hiari katika kambi ya uchunguzi, upimaji, tiba na ushauri wa afya zinazotolewa kwa watumishi wote wa Wizara na Taasisi za Umma.
Kambi hiyo inayoendeshwa na Wataalam wa Afya kutoka Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa inafanyika katika Jengo dogo la zamani la Ofisi ya Rais-UTUMISHI lililopo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Baadhi ya huduma zinazotolewa katika kambi hiyo ni pamoja na Saratani, Tiba Ukunga na Magonjwa ya akina Mama, Magonjwa ya Figo, Moyo, Macho, Masikio, Pua, Koo, Mifupa na Ajali
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeshirikiana na Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa katika kuratibu zoezi hilo ikilenga kuwafikia watumishi wa umma ili waweze kufahamu hali zao za afya na kupata ushauri wa kitaalam kutoka kwa Madaktari Bingwa.