Habari
WATENDAJI SERIKALINI WAJENGEENI UWEZO WATUMISHI WENU ILI KUTATUA CHANGAMOTO YA UPUNGUFU WA WATAALAM -MHE. JENISTA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Halmashauri ya Mji Mbinga na taasisi nyingine za Serikali mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyasa ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mhe. Kanali Laban Thomas na kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma, Bw. Stephen Ndaki.