Habari
WASHIRIKI WA KIKAO KAZI CHA KUTATHMINI MATOKEO YA UTAFITI WA HALI YA UZINGATIAJI WA MAADILI WATAKIWA KUTOA MAPENDEKEZO YATAKAYOIMARISHA UADILIFU KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika kikao kazi cha wadau wa usimamizi wa maadili katika utumishi wa umma kilicholenga kujadili matokeo ya tafiti ya hali ya uzingatiaji maadili katika utumishi wa umma ya mwaka 2022 kabla ya kufungua kikao kazi hicho jijini Dodoma. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Bi. Leila Mavika.