Habari
WANAWAKE WA OFISI YA RAIS, UTUMISHI NA UTAWALA BORA WAUNGANA NA WANAWAKE WENGINE MKOANI DODOMA KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Watumishi Wanawake wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wameungana na wanawake wengine jijini Dodoma na Duniani kote kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 08 kila mwaka.
Watumishi hao wameongozwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi hiyo, sehemu ya Utawala, Bi Mwalibora Mwamtuya katika kuadhimisha Siku hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Chinangali kwa ngazi ya Mkoa, jijini Dodoma.
Maadhimisho hayo Kitaifa yamefanyika Jijini Arusha ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni ‘’ Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji" Lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kukuza Usawa, Haki na Uwezeshaji wa Wanawake na Wasichana kwa kuzingatia kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 ili wajiamini, wajiandae na wajitokeze kugombea nafasi za uongozi.