Habari
WANAWAKE OFISI YA RAIS-UTUMISHI WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2025

Watumishi Wanawake kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wameshiriki kwa wingi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 8, 2025 jijini Arusha ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wanawake ni jeshi kubwa ambalo likiwezeshwa katika masuala mbalimbali nchini huongeza chachu ya utendaji kazi kwa kuzingatia usawa wa kijinsia kwa kushirikiana na wanaume na kuleta maendeleo kwa ustawi wa taifa.
Katika kuadhimisha Siku hiyo, Wanawake wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI walipata fursa ya kishiriki kikamilifu maonesho kuanzia tarehe 01 Machi hadi 08 kwenye Kilele cha Maadhimisho hayo kwa kutoa huduma mbalimbali za Kiutumishi kwa Watumishi wa Umma na Wananchi.
Maadhimisho hayo kwa Mwaka huu yamefanyika Kitaifa Jijini Arusha katika Viwanja vya Amri Abeid Karume yaliyobeba kauli mbiu isemayo “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji”.