Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

WANANCHI WAHIMIZWA KUJITOKEZA KWA WINGI KILELE CHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2026


Wananchi wa Mkoa wa Dodoma na maeneo ya jirani wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kesho, Juni 23, 2026, kushiriki kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2026 yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

Aidha, ushiriki wao utasaidia kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali pamoja na kujionea mafanikio yaliyofikiwa katika sekta ya utumishi wa umma.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray, baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya Wizara na Taasisi za Umaa zinazoshiriki maadhimisho hayo.

Mhe. Regina amesema maadhimisho hayo yamekuwa fursa muhimu kwa wananchi kupata huduma za papo kwa papo, ushauri na elimu kuhusu majukumu na huduma zinazotolewa na Serikali katika sekta mbalimbali.

Aidha, amezipongeza Wizara na Taasisi za Umma kwa juhudi kubwa wanazoendelea kufanya katika kutoa huduma na elimu kwa wananchi kupitia mabanda ya maonesho, hali ambayo imeongeza uelewa wa wananchi kuhusu huduma za Serikali na namna ya kuzifikia kwa urahisi.

Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2026 kitafanyika kesho, Juni 23, 2026