Habari
WALENGWA WA TASAF KATA YA RUSIMBI KIGOMA UJIJI WATAKIWA KUBORESHA MAISHA YAO ILI KUTOMUANGUSHA MHE. RAIS BAADA YA KUONGEZA MUDA WA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA TASAF

Wananchi wa Kata ya Rusimbi, Mtaa wa Kawawa na Taifa mkoani Kigoma wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (Wakwanza kulia) wakati akizungumza nao alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.