Habari
WAKAZI WA MAJANI YA CHAI JIJINI TANGA WAPONGEZWA KUKIPAMBANIA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA KUPATA KIWANJA CHA KUJENGA KAMPASI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wananchi wa Majani ya Chai kata ya Maweni jijini Tanga alipoenda kuwatembelea kwa lengo la kuwashukuru kwa jitihada zao za kukiunga mkono Chuo cha Utumishi wa Umma kupata hati ya kumiliki kiwanja kwa ajili ya kujenga kampasi ya chuo hicho jijini humo.