Habari
WAAJIRI TATUENI CHANGAMOTO YA UHABA WA WATUMISHI KWA KUBAINI NA KUWAENDELEZA WATUMISHI WENYE UJUZI ILI KUZIBA NAFASI KATIKA KADA ZENYE UHITAJI

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi (katikati) akisikiliza hoja iliyokuwa ikiwasilishwa na Mtumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa hiyo. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Nyangasa na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Bw. Erasto Kiwale.