Habari
WAAJIRI SERIKALINI WATAKIWA KUTOKWEPA JUKUMU LA KUWACHUKULIA HATUA WATUMISHI WANAOKIUKA MAADILI

Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Ufuatiliaji wa Uzingatiaji wa Maadili, Bi. Janeth Mishinga akiwasilisha maazimio yaliyopendekezwa na wadau wa usimamizi wa maadili katika utumishi wa umma kabla ya Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi kufunga kikao kazi cha wadau hao cha siku mbili kilicholenga kujadili matokeo ya tafiti ya hali ya uzingatiaji maadili katika utumishi wa umma ya mwaka 2022, jijini Dodoma.