Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

WAAJIRI SERIKALINI WATAKIWA KUTOKWEPA JUKUMU LA KUWACHUKULIA HATUA WATUMISHI WANAOKIUKA MAADILI


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akisikiliza maazimio ya kikao kazi cha siku mbili cha wadau wa usimamizi wa maadili katika utumishi wa umma kilicholenga kujadili matokeo ya tafiti ya hali ya uzingatiaji maadili katika utumishi wa umma ya mwaka 2022 jijini Dodoma. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa kikao kazi hicho, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mipango Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Cosmas Ngangaji na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Bi. Leila Mavika.