Habari
VIONGOZI WA SERIKALI ZA VIJIJI WAHIMIZWA KUWEKA UWAZI KATIKA KUWATAMBUA WANAOSTAHILI KUINGIZWA KWENYE MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI ILI KUEPUSHA MALALAMIKO

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi na walengwa wa TASAF wa Kata ya Masaki, Kijiji cha Kisanga katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.