Habari
UTUMISHI YAENDELEA KUNG'AA, YAINGIA NUSU FAINALI MPIRA WA PETE

Timu ya Mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais UTUMISHI imeendelea kuonyesha umahiri wake katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) baada ya kufuzu kuingia hatua ya Nusu Fainali Septemba 10, 2025 jijini Mwanza.
Utumishi imefanikiwa kutinga hatua hiyo kwa kuibuka na ushindi wa kishindo dhidi ya wapinzani wao ambao ni timu ya Mahakama kwa magoli 80 kwa 18, jambo linaloendelea kuthibitisha ubora na maandalizi ya timu hiyo katika mashindano ya mwaka huu.
Mashabiki na watumishi wa ofisi hiyo wameendelea kuipongeza timu kwa mshikamanio na nidhamu kubwa waliyoionyesha ndani na nje ya uwanja, wakisisitiza matumaini makubwa ya kutwaa ubingwa wa SHIMIWI 2025.
Kwa hatua hiyo, timu ya Utumishi sasa inasubiri kuivaa mpinzani wake ambaye ni timu ya mpira wa pete ya Ikulu katika mchezo wa Nusu Fainali unaotarajiwa kuchezwa Septemba 13, 2025 kuvutia mashabiki wengi kutokana na kiwango bora walichokionesha.