Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

“TUENDELEZE USHIRIKIANO ILI KUJENGA UTUMISHI WA UMMA ULIOTUKUKA” BW. XAVIER DAUDI ASISITIZA


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi ametoa wito kwa baadhi ya wakurugenzi wa Idara za Ofisi yake pamoja na Ofisi ya Rais, Katiba Sheria na Utawala Bora ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendeleza ushirikiano uliopo ili kuleta mageuzi na kujenga Utumishi wa Umma uliotukuka kwa ustawi wa Taifa.

Bw. Daudi ameyasema hayo leo tarehe 15 Januari, 2026 wakati akimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi katika kikao cha kubadilishana uzoefu wa utekelezaji wa majukumu ya kiutumishi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi hiyo uliyopo Mtumba jijini Dodoma.

“Ili kujenga na kuboresha Utumishi wa Umma wenye tija ni vizuri tukashirikiana wenyewe kwa wenyewe hasa kwa yale mazuri tuliyo nayo ndani ya muungano” Bw. Xavier alisema.

Nae Naibu Katibu Mkuu Utumishi na Utawala Bora Bw. Omar Haji Gora ameushukuru uongozi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI chini ya Katibu wake Mkuu Bw. Juma Mkomi kwa Kuwaonesha ushirikiano kila wakati na kuahidi kuwa yale yote waliyojifunza wataenda kuyafanyia kazi ili kuleta mageuzi katika Utumishi wa Umma.

“Tumepata faraja kuwa hapa, na yale ambayo tumejifunza tunaenda kuyafanyia kazi ili kuendelea kujenga utumishi wa umma ulio Bora” Bw. Gora alisema.