Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YAIPONGEZA TGFA


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama kwa niaba ya Wajumbe wa kamati hiyo ameipongeza Wakala wa Ndege za Serikali kwa utendaji uliotukuka na unaozingatia misingi na maadili ya utumishi wa umma wakati wote.

Mhe. Mhagama amesema hayo tarehe 2 Septemba, 2023 wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo katika Ofisi za Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) jijini Dar es Salaam.