Habari
TASAF YATEKELEZA MAELEKEZO YA MHE. RAIS YA KUJENGA BARABARA KWA GHARAMA NAFUU KIJIJI CHA NANGOSE AMBAZO HAZIKUWAHI KUJENGWA TANGU TAIFA LIPATE UHURU

Sehemu ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na Wananchi wa Kijiji cha Nangose Kata ya Temeke Halmashauri ya Mji Masasi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilayani Masasi.