Habari
TASAF YAELEKEZWA KUJENGA WODI YA AKINA MAMA NA AKINA BABA KATIKA ZAHANATI YA LUSHAMBA ILI KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akisikiliza hoja ya mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Kijiji cha Lushamba, Kata ya Bulyaheke, Halmashauri ya Buchosa, wilayani Sengerema alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo mkoani Mwanza.