Habari
TASAF KUJENGA JENGO JIPYA LA KUTOA HUDUMA ZA KITABIBU KATIKA KITUO CHA AFYA CHA DONGE VIJIBWENI ZANZIBAR

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi na wanufaika wa TASAF wa Shehia ya Donge Pwani iliyopo Wilaya ya Unguja Kaskazini B, mara baada ya waziri huyo kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar.