Habari
TANZANIA KUSHIRIKIANA NA AZERBAIJAN KUBORESHA UTOAJI WA HUDUMA KWA WANANCHI

Mwenyekiti wa Wakala wa Taifa kwa Utumishi wa Umma na Ubunifu wa Kijamii ya nchini Azerbaijan, Mhe. Ulvi Mehdiyev akizungumza jijini Dar es Salam mara baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kufanya kikao cha pamoja na timu ya wataalamu kutoka nchini Azerbaijan kwa ajili ya kubadilishana uzoefu katika utoaji wa huduma bora na ya pamoja ‘‘ One Stop Service Center” kwa wananchi kufuatia nchi hiyo kupiga hatua kubwa katika eneo hilo.