Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

TANGAZO LA MNADA WA HADHARA


 

 

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inapenda kuwaalika wananchi wote kwenye mnada wa hadhara wa vifaa chakavu. Lengo la Mnada huo ni kuuza vifaa chakavu Vya Tehama, Vifaa na Samani za Ofisi. Mnada huo utafanyika katika ofisi za Utumishi zilizoko Dodoma na Dar es Salaam kama ilivyooneshwa katika jedwali lifuatalo.

Tarehe ya Mnada
6/6/2025
Sehemu Mali Ilipo: Kivukoni-Dar es Salaam

Vifaa vya Tehama (Printer, scanner, UPS, Computer, CPU, Keyboard, Photocopier, switch)
Vifaa vya Ofisi (File cabinet 4drawers, Microwave, Paper shredder, Decorder startimes, Telephone receiver, Water dispenser, Binding machine,)
Samani za ofisi (Office Chair, TV Stand LG, Table Steel, Table parts, Office table, Miguu ya meza wooden, Sofa, bookshelf)

Tarehe ya Mnada 13/6/2025
Sehemu Mali Ilipo: Mji Wa Serikali Mtumba-Dodoma

Vifaa vya Tehama (Printer, scanner, UPS, Computer, CPU, Keyboard, Photocopier na switch)
Vifaa vya Ofisi (File cabinet 4drawers, Microwave, Paper shredder, Decorder startimes, Telephone receiver,Water dispenser, Television Sony, Binding machine,)
Samani za ofisi (Office Chair, TV Stand LG, Table Steel, Table parts, Office table, Miguu ya meza wooden, Sofa, bookshelf)


Masharti ya Mnada

1. Mnada saa nne(4:00) asubuhi katika kila kituo
2. Mali zote zitauzwa kama zilivyo na mahali zilipo
3. Mnunuzi atatakiwa kulipa asilimia mia moja(100%) ya bei ya kifaa atakachonunua papo hapo siku ya 
mnada
4. Mnunuzi atatakiwa kuhamisha kifaa atakachonunua ndani ya siku ya mnada
5. Ruhusa ya kuangalia mali itatolewa siku moja (1) kabla ya tarehe ya mnada

NYOTE MNAKARIBISHWA

IMETOLEWA NA KATIBU MKUU OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA
26 MEI, 2025.