Habari
TAASISI YA UONGOZI INATOA MAFUNZO YANAYOWAJENGEA UWEZO VIONGOZI KIUTENDAJI ILI KUIMARISHA UTAWALA BORA NCHINI

Sehemu ya washiriki wa Awamu ya Tatu ya Programu ya Mafunzo kwa Viongozi yanayoratibiwa na Taasisi ya UONGOZI kwa kushirikiana na Serikali ya Finland na Umoja wa Mataifa wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati akizindua mafunzo hayo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.