Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

SHUKURANI KWA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amefurahia na kushukuru kwa ujio wa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na katika Ofisi za Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA).

“Ujio wenu hapa unaambatana na maelekezo muhimu sana kwetu ili kuimarisha shughuli zinazofanywa na Wakala hii kwa ustawi wa Serikali na Taifa kwa jumla” alisema Mhe. Simbachawene.

Alisema hayo wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo katika ofisi za TGFA zilizopo jijini Dar es Salaam, tarehe 2 Septemba, 2023.