Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

SERIKALI YAZIDI KUWAPANDISHA VYEO  MAELFU YA WATUMISHI 


 

 Serikali imesema kwamba katika Mwaka wa Fedha 2022/2023 imewapandisha vyeo watumishi 180,000 wakiwemo watumishi walioathirika na mwongozo wa upandaji madaraja wa miaka minne.

Mhe. Sangu amesema hayo  wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.  Janejelly Ntate  aliyetaka kujua Serikali imejipangaje kukwamua watumishi walioathiriwa na mwongozo wa upandaji madaraja wa miaka minne.


Aidha, katika utekelezaji wa Ikama na Bajeti ya Mwaka 2023/2024, Serikali imewapandisha vyeo watumishi zaidi ya 232,530 wakiwemo walioathirika
na zoezi hilo, uhakiki wa vyeti feki na watumishi hewa