Habari
SERIKALI YAWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUWA WAADILIFU
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi amewataka watumishi wa Ofisi yake kuzingatia sheria na kanuni za maadili ya utumishi wa umma na kutumia ujuzi wa kitaaluma walionao ili kutoa huduma bora kwa umma.
Bw. Mkomi ameyasema hayo wakati akihitimisha mafunzo ya kila wiki ya kuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora yaliyofanyika katika eneo maalumu la Ofisi hiyo lililopo Mtumba jijini Dodoma.
“Naomba nitoe rai kwenu kuwa kila mtumishi wa Umma kwa nafasi yake ahakikishe anatekeleza majukumu yake kwa uwazi, uaminifu, weledi na ufanisi ili kuepusha malalamiko ya wananchi kwa Serikali” alisema Bw. Mkomi.
Vile vile Bw. Mkomi amezishukuru na kuzipongeza Kurugenzi husika zilizoandaa mada pamoja na watoa Mada kwa uwasilishaji wao mzuri ambao umetoa uelewa utakaoboresha utendaji kazi wa watumishi wa umma.
Awali, Mchambuzi Kazi Mwandamizi kutoka Idara ya Uendelezaji Taasisi Bw. MacDonald Kiwis wakati akiwasilisha mada ya Uandishi wa Nyaraka za Serikali alisema kuwa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Taasisi zote za Umma kwa jumla hazina budi kufuata miongozo ya uandishi wa nyaraka za Serikali ili kuwa na viwango vinavyofanana.
Naye Afisa Rasilimaliwatu Mwandamizi kutoka Idara ya Usimamizi wa Maadili Bw.Hassan Kilenza akiwasilisha mada ya Utambuzi wa Watoa Mrejesho alisema kuwa watumishi wa umma wanatakiwa kutoa mrejesho kwa wateja wakizingatia taratibu na uwepo wa takwimu sahihi ili kuepuka uwepo wa taarifa zisizofanan
