Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

SERIKALI KUCHUKUA HATUA KWA WATUMISHI WA UMMA WANAOKIUKA MAADILI


 

Serikali imesema itaendelea kuchukua hatua dhidi ya watumishi wa umma wanaothibitika kukiuka maadili ya utumishi wa umma  huku  ikiahidi kuwekeza zaidi katika matumizi ya TEHAMA ili kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa Maadili

 

Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bw.Juma Mkomi  ametoa kauli hiyo leo  jijini Dodoma wakati akifunga Kikao kazi cha kubadilishana  uzoefu  wa masuala ya Maadili na Utawala Bora  baina ya Taasisi  Simamizi  za Maadili ya Utendaji na Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma.

 

Amesema watumishi wala rushwa na walevi na wenye tabia na mienendo isiyofaa kwenye jamii  haitawafumbia macho

 

‘’Hivi karibuni nimewahamisha watumishi wanne kutoka wizara fulani  wanaotuhumiwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja.

 

‘’ Kuna baadhi ya  watumishi wanalala baa na asubuhi wanakwenda kazini wakiwa wachovu na hawajapiga mswaki na hivyo kuwapa shida wananchi wanapowahudumia’’ ameng’aka  Katibu Mkuu Mkomi

 

Amesema dhana ya utumishi wa umma ni maadili na bila maadili hakuna utumishi wa umma hivyo Serikali itaendelea kufanya tahtmini kwa kina kuhusu tabia na mienendo ya watumishi wa umma  wakati wote.

 

Kufuatia hatua hiyo Mkomi amesema   watumishi wapya watakaokuwa wakiajiriwa  wataanza  kufanyiwa upekuzi wa kutosha   kuhusu tabia na mienendo yao kulingana na majukumu na miiko ya taaluma zao ili kuwa na utumishi wenye taswira nzuri

 

Katika hatua nyingine Mkomi amewataka Waajiri  kuimarisha mifumo madhubuti na taratibu za kuwalinda watoa taarifa juu ya vitendo vya ukiukwaji wa maadili na rushwa mahali pa kazi

Amesema kumeibuka tabia za baadhi ya waajiri kushindwa kuwalinda watoa taarifa pindi mnapoletewa taarifa ya vitendo vya ukiukwaji maadili, hii sio sawa walindeni hao ni watu muhimu