Habari
RAIS KAGAME AWASILI TANZANIA KUSHIRIKI MKUTANO WA KUJADILI AMANI YA DRC

Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame amewasili nchini Tanzania kwa ajili ya mkutano wa kujadili amani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC),
Mhe. Kagame amewasili asubuhi ya leo Jumamosi Februari 8, 2025 na kupokewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Mkutano huo unafanyika huku vikundi vya waasi chini ya Alliance Fleuve Congo (AFC/M23) vimekamata miji ya Goma, Kivu Kaskazini na Nyabibwe, Kivu Kusini vikielekea Bukavu.