Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (Wa tatu kutoka kushoto) akiwasili katika Uwanja wa Jamhuri kwa ajili ya uzinduzi wa bonanza la michezo ya SHIMIWI lililofanyika leo jijini Dodoma. Wa pili kutoka kulia ni Katibu Mkuu-IKULU, Bw. Mululi Majula Mahendeka. Wengine ni Viongozi wa Serikali waliohudhuria bonanza hilo.