Habari
OFISI YA RAIS-UTUMISHI, WIZARA YA FEDHA NA WATUMISHI HOUSING INVESTMENTS YAKAGUA MIRADI YA UJENZI WA MAKAZI YA WATUMISHI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA MKOANI RUVUMA

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (aliyenyoosha mkono) akizungumza jambo na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mipango na Bajeti, Bi. Julieth Magambo (wakwanza kulia) mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Umma yanayojengwa katika Kituo cha Afya Kilagano, Halmashauri ya Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma. Wapili kutoka kulia ni Mteknolojia wa Maabara-Kituo cha Afya Kilagano, Bw. Lugano Mwakalago.