Habari
NYUMBA ZA WATUMISHI WA KITUO CHA AFYA NYABILEZI ZIMEJENGWA NA TASAF KUWAWEZESHA WATUMISHI KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akielekea kukagua ujenzi wa nyumba za watumishi katika kituo cha afya cha Nyabilezi (Nyabilezi Health Centre) kilichopo wilayani Chato wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Geita, wengine ni watendaji wa mkoa huo.