Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

MTANDAO WA WABUNGE WA KUPAMBANA NA RUSHWA AFRIKA TAWI LA TANZANIA KUSHIRIKIANA NA TAKUKURU KUITOKOMEZA RUSHWA NCHINI


Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na Rushwa Afrika tawi la Tanzania (APNAC) Mhe. Cecilia Pareso (Mb) akizungumza wakati wa semina kuhusu elimu ya mapambano dhidi ya rushwa iliyoandaliwa na TAKUKURU jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo wajumbe wa mtandao wa APNAC ili waweze kushirikiana vema na TAKUKURU katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.