Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

MSITUME NYARAKA ‘WHATSAPP’ Ni MARUFUKU


 

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema sheria inayosimamia nyaraka za Serikali inaelekeza kuwa mawasiliano ya Serikali yafanyike kwa njia ya barua na si vinginevyo.

Kufuatia kuwepo kwa sheria hiyo, Naibu Waziri  Kikwete  amewaonya watendaji wa Serikali ambao  wanatumia njia ambazo sio rasmi kutuma nyaraka. 

“Haitokuwa sawa na ni marufuku ya Serikali kuwasilisha au kutumiiana ‘Documents’ za Serikali kupitia njia ya WhatsApps na njia nyingine zisizo rasmi, isipokuwa kwa maelekezo ambayo yatakuwa yametolewa vinginevyo katika mamlaka,” amesema Naibu Waziri Ridhiwani Kikwete.

Ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Janejelly Ntate James ambaye amehoji uhalali wa  matumizi ya makundi ya WhatsApp kutumiana nyaraka. 

Aidha, Naibu Waziri Kikwete amelihakikishia Bunge kuwa  Serikali bado inaendelea kutengeneza mifumo mbalimbali ambayo itaileta ufanisi katika utendaji kazi Serikalini.