Habari
MKUU WA MKOA WA DODOMA MHE. SENYAMULE ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA RAIS-UTUMISHI

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule leo Alhamisi Machi 07, 2024 ametembelea Banda la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo katika Viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma ambako Maonesho ya Wiki ya Wanawake yanafanyika kwa muda siku tano kuanzia leo.
Mhe. Senyamule pamoja na mambo mengine ameipongeza Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa kushiriki katika Maonesho hayo huku akiitaka itoe huduma nzuri kwa Watanzania ili kukidhi ndoto ya Rais Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuwahudumia Watanzania wote kwa usawa.
Tanzania inaungana na nchi nyingi Duniani katika kuadhimisha Kilele cha Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika kila mwaka Machi 8, 2024 kwa kuthamini na kutambua mchango wa wanawake katika ujenzi wa jamii na taifa bora kiujumla