Habari
MKURUGENZI OFISI YA RAIS UTUMISHI AAGWA RASMI
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Taasisi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Nolasco Kipanda kwa niaba ya Katibu Mkuu na Watumishi wote wa Ofisi hiyo amemuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu wa Ofisi hiyo Bi. Mariam Mwanilwa ambaye amestaafu kwa kwa mujibu wa Sheria.
Bw. Kipanda ameyasema hayo Aprili 27, 2026 katika eneo maalum la mafunzo lililopo katika ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma.
Amesema, Ofisi ya Rais-Utumishi itamkumbuka Mkurugenzi huyo kwa upendo wake, umahiri, ujasiri, mchango na kazi nzuri aliyoifanya ya kuleta tija katika utumishi wa Umma.
Kwa upande wake, Bi. Mwanilwa amewaasa watumishi hao kufanya kazi kwa umoja na kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma ili kutoa huduma kwa haki na usawa.
Bi. Mwanilwa aliwasisitiza watumishi wa umma kufanya kazi kwa kujituma huku wakizingatia maadili ya utendaji ili kuufikia mwisho mwema wa utumishi wao.
