Habari
MHE. SIMBACHAWENE ARIDHISHWA NA THAMANI YA FEDHA ILIYOTUMIKA KATIKA MRADI WA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA MWANANGWA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MISUNGWI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akimsikiliza Mkurugenzi wa Miradi ya Jamii-TASAF, Bw. John Stephen alipokuwa akifafanua jambo kwa Waziri huyo mara baada ya kukagua Shule ya bweni la wasichana Mwanangwa lillojengwa kwa ufadhili wa TASAF katika Kijiji cha Mwanangwa, wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.